Kitaifa

Jumatatu, 12 Septemba 2016

Arsene Wenger: Naimani Jack Wilshere atasalia Arsenal maisha yake ya uchezaji

Kocha Arsene Wenger amesema anamatumaini ya kiungo wake wa kati Jack Wilshere, ambaye kwa sasa yupo klabu ya Bournemouth kwa mkopo, atasalia Arsenal maisha yake ya uchezaji
Wilshere, 24, ambaye huchezea timu ya taifa ya Uingereza, alienda Bournemouth kwa mkopo wa msimu mmoja.
Ni mmoja wa wachezaji waliokua kutoka chuo cha kustawisha wachezaji cha Arsenal na aliwachezea mechi yake ya kwanza 2008 akiwa na miaka 16.
Lakini alicheza mechi tatu pekee klabu hiyo msimu uliopita kutokana na majeraha.
“Yeye ni mchezaji stadi sana, hahitajiki kufanya jambo jingine kunionyesha uwezo wake,” amesema Wenger.
“Binafsi, natumai atasalia hapa maisha yake yote ya uchezaji.”
Wenger amesema walizungumza na mchezaji huyo.
Bournemouth watakutana na West Bromwich Albion leo Jumamosi na Wilshere anatarajiwa kucheza




Hakuna maoni:

Chapisha Maoni