Kitaifa

Jumatatu, 24 Oktoba 2016

Yanga yapangua benchi zima la ufundi

Hatimaye klabu ya yanga imevunja mkataba wake na aliekuwa kocha wao mholanzi Hans van de pluim maarufu Ka babu .Yanga imefikia uamuz huo baada ya kutoridhishwa na matokeo ya timu hyo katika ligi wengine waliotimuliwa kocha msaidizi juma mwambusi,juma pondamali kocha wa makipa na meneja afidhi salehe chanzo kinasema mpaka sasa George Lwandamina kutoka Zambia kashawasili na kusaini kandarasi ya miaka miwili na kufanikiwa kumrejesha mkwasa kama kocha msaidizi ,upande wa kocha wa golikipa ni manyika Peter na meneja ni Sekilojo Chambua awali George Lwandamina alikuwa akiinoa Zesco united ya Zambia

Leo ni birthday ya bosi wa Chelsea

Leo ni birthday ya mmliki wa klabu ya Chelsea Roman Abrahimovic ambaye anafikisha miaka kadhaa

Jumatatu, 12 Septemba 2016

Arsene Wenger: Naimani Jack Wilshere atasalia Arsenal maisha yake ya uchezaji

Kocha Arsene Wenger amesema anamatumaini ya kiungo wake wa kati Jack Wilshere, ambaye kwa sasa yupo klabu ya Bournemouth kwa mkopo, atasalia Arsenal maisha yake ya uchezaji
Wilshere, 24, ambaye huchezea timu ya taifa ya Uingereza, alienda Bournemouth kwa mkopo wa msimu mmoja.
Ni mmoja wa wachezaji waliokua kutoka chuo cha kustawisha wachezaji cha Arsenal na aliwachezea mechi yake ya kwanza 2008 akiwa na miaka 16.
Lakini alicheza mechi tatu pekee klabu hiyo msimu uliopita kutokana na majeraha.
“Yeye ni mchezaji stadi sana, hahitajiki kufanya jambo jingine kunionyesha uwezo wake,” amesema Wenger.
“Binafsi, natumai atasalia hapa maisha yake yote ya uchezaji.”
Wenger amesema walizungumza na mchezaji huyo.
Bournemouth watakutana na West Bromwich Albion leo Jumamosi na Wilshere anatarajiwa kucheza